Unaalikwa kwa Karamu ya “Njoo Ulivyo”

Unaalikwa kwa Karamu ya “Njoo Ulivyo”

Ambaye katika yeye tulipokea neema…ambao katika hao ninyi mmekuwa wateule wa Yesu Kristo. WARUMI 1:5–6

Mojawapo ya vitu vya kwanza ambavyo huwa tunauliza tukialikwa kwenye karamu ni, “Nitavaa vipi?” Wengi wetu hupenda tukihisi kwamba tunaweza kuja jinsi tulivyo. Tunapenda wakati ambao tunaweza kutulia na kuwa sisi. Ninapenda Andiko hili kwa sababu ya ujumbe wa ukubalifu linaloleta.

Mungu hutukubali jinsi tulivyo na hufanya kazi nasi katika maisha yetu yote ili kutusaidia kuwa yote ambayo anataka tuwe. Neema hukutana nasi tulipo lakini, shukuru kwamba huwa haituachi ilipotupata.
Mungu atafanya kazi ndani yako kwa Roho Mtakatifu na utabadilishwa! Lakini huna haja ya kungoja ili uje kwake. Shukuru kwamba unaweza kuja sasa hivi. Huhitaji kusimama mbali na kusikia tu muziki wa karamu; umealikwa kuhudhuria.


Sala ya Shukuru

Ninakushukuru, Baba, kwamba unanipenda vile tu nilivyo. Ninajua kuwa unafanya kazi maishani mwangu ili kuleta mabadiliko chanya, lakini ninakushukuru kwamba ungali unanipenda na kunikubali katika mchakato huo. Asante kwa neema yako inayoniruhusu kuja kwako tu jinsi nilivyo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon