nzuri ya kutosha

nzuri ya kutosha

Naye atayachukua maovu yao. Isaya 53:11

Kwa wengi wetu, shida yetu kubwa ni kwamba hatujipendi sisi wenyewe, na mtazamo wetu usiofaa hufanya iwe vigumu kuamini kwamba Mungu anaweza kutupenda. Kwa miaka mingi nilikuwa na shida hii.

Nilitumia angalau asilimia 75 ya wakati wangu nikijaribu kujibadili mwenyewe, lakini yote niliyoyafanya ilikuwa kujisumbia kila wakati wakati huku shetani akifanya nijisikie mwenye hatia. Sikujawahi kujisikia vizuri.

Isaya 53 inatuambia kwamba wakati Yesu alipokufa kwa ajili ya dhambi zetu, pia alichukuwa na hatia zetu. Yeye alitupenda sana kiasi kwamba alilipa bei ili tusiwe na hisia za kutisha za hukumu. Ikiwa tunamwendea Mungu na kumwomba kwa dhati atusamehe, Yeye hufanya hivyo, basi hakuna sababu ya kuishi na hukumu.

Mungu anakupenda, na anataka uamini na upokee upendo wake wakati wote. Anataka pia kukuweka huru kutokana na hatia na hukumu. Mungu anasema wewe ni mzuri wa kutosha. Kubali hayo leo na uishi maisha ya ushindi.

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, Mwana wako amechukua hatia yangu na adhabu na kupitia Kristo, mimi ni mzuri wa kutosha. Ninaamini leo, na mimi nakataa kuishi na mzigo wa hatia na hukumu. Ninaomba na kupokea msamaha wako kwa ajili ya dhambi zangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon