Omba na Usiogope

Omba na Usiogope

Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi. — 2 TIMOTHEO 1:7

Mungu anataka tuombe kuhusu kila kitu na kutoogopa chochote. Tutajipata katika uhusiano wa kibinafsi wa ndani na karibu na Bwana iwapo tutaomba zaidi, kutokuwa na mawazo na kutokuwa na hofu. Timotheo anasema kwamba Mungu hajatupatia roho ya woga. Kwa hivyo tukihisi woga, hautakuwa unatoka kwa Mungu. Unatoka kwa shetani. Shetani atajaribu kututisha kwa kila aina za woga, na tunaweza kuwaza sana kuhusu vile tunavyohisi tukasahau kuomba.

Iwapo Ibrahimu au Yoshua au Daudi wangeupigia magoti woga kazi iliyokuwa mbele yao ilipoonekana kuwa nyingi, wasingemwona Bwana kama anayetimiza mahitaji yao kwa wingi.

Kuzungumza na Mungu na kutumia muda katika Neno lake hukupa nguvu za kupinga woga unapokuja. Unapotia Neno la Mungu katika moyo wako, litatoka utakapolihitaji. Ninaamini tunafaa kukiri Neno la Mungu kwa sauti na kujaza maombi yetu kwa Neno al Mungu. Huenda shetani asikuogope, lakini anaogopa Neno la Mungu lililonenwa kwa imani kutoka kwa kinywa cha aaminiye.

Woga hauwezi kupuuzwa, lazima ukabiliwe. Maombi na Neno la Mungu ni silaha zetu mbili zilizo na nguvu sana, kwa hivyo acha tuzitumie!


Vaa silaha za Mungu kupitia kwa maombi na kusimama kinyume na mishale yenye moto ya woga kutoka kwa adui.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon