Omba Neno

Ee Bwana Neno lako lasimama imara mbinguni hata milele (ZABURI 119:89)

Unajua kwamba Mungu hutuzungumzia kupitia kwa Neno lake. Tunaweza kumzungumzia Neno lake tunapoomba kwa “kuomba Neno.” Pengine hujawahi kusikia msemo “omba Neno” na unashangaa jinsi utakavyofanya hivyo. Ninafikiri “kuomba Neno au kuomba maandiko,” jinsi watu wengine wanavyosema, ndio utaratibu rahisi sana wa maombi ambao kila aaminiye anao. Kinachofanyika ni kwamba, unasoma au kukariri maneno katika Biblia na kuomba kwa njia ambayo inayafanya yawe yako binafsi au kuyatumia kwa ajili ya mtu mwingine. Ninaamini njia nzuri ya kufanya hivi ni kunukuu maandiko kwa kusema, “Mungu, Neno lako linasema (weka andiko) na ninaliamini.”

Iwapo ulikuwa unajiombea Yeremia 31:3, ungesema kitu kama hiki: “Mungu, Neno lako linasema kwamba umenipenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.” Ninakushukuru kwa kunipenda sana na kuendelea kunivuta karibu nawe kwa fadhili kama hizo.  “Nisaidie Bwana, kufahamu na kujua upendo ulio nao kwangu.” Iwapo ulikuwa unamwombea andiko hilo rafikiyo Susie ambaye amekuwa aking’ang’ana kuamini kwamba Mungu anampenda kweli, utasema kitu kama hiki, “Mungu, Neno lako linasema kwamba umempenda Susie kwa upendo wa milele na kwamba umemvuta kwa fadhili zako. Mungu, unajua kwamba Susie hajahisi usalama katika upendo wako hivi karibuni, kwa hivyo ninakuomba uinuke juu ya hisia zake kwa ukweli wa ahadi hii.”

Ahadi za Mungu ni zako wewe; ni za kila aaminiye- na anapendezwa tunapojua Neno lake.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Mungu anakupenda jinsi ulivyo na atakusaidia kuwa anachotaka uwe.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon