Pokea Msamaha na Usahau Dhambi Zako

Pokea Msamaha na Usahau Dhambi Zako

. . . Maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena. —YEREMIA 31:34

Haijalishi shida uliyo nayo au vile unavyohisi kujihusu kwa sababu ya shida hiyo, Mungu anakupenda na anataka kuwa katika uhusiano wa karibu nawe. Ndani ya Yesu, amekupa maisha mapya. Atakupa familia mpya ya marafiki Wakristo kukupenda, kukukubali, kukufurahia na kukusaidia. Utafurahia maisha ya ushindi kwa sababu ya Yesu, anayeishi ndani yako na kukujali.

Unapotenda dhambi unaweza kutubu na kupokea msamaha. Mungu anapokuonyesha dhambi yoyote katika maisha yako, kubaliana naye tu na ushangazwe na wema wake. Mungu hatusamehi tu, lakini anaahidi kusahau dhambi yetu.

Rehema ya Mungu ni ajabu na tunapopokea upendo wake, msamaha na rehema, tunaweza pia kujifunza vile tunavyoweza kuwapa watu wengine wanaotudhuru na kutusikitisha katika maisha yetu. Ukiwa na hasira na mtu yeyote, ninapendekeza umwonyeshe rehema huyo mtu ambaye Mungu amekupa. Kadri unavyoruhusu upendo kuja kwako kutoka kwa Mungu na kupitia kwako hadi kwa wengine, ndivyo utafurahia zaidi.


Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi. Tunaweza kupata mahali papya pa kuanzia kila siku.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon