Roho wa Kuasili

Roho wa Kuasili

Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba! —WARUMI 8:15

Mtume Paulo anatufundisha kwamba Roho Mtakatifu ni Roho wa kuasili. Neno kuasili linamaanisha kwamba tumeletwa katika familia ya Mungu, ingawa awali tulikuwa watu wa nje, bila uhusiano na Mungu. Tulikuwa watenda dhambi, tukiwa mbali na Mungu, lakini Mungu kwa rehema yake kuu, alitununua, na kutuleta karibu naye tena kupitia kwa damu ya Mwanawe.

Tunafahamu kuasiliwa kwa maana yake ya kiasili. Tunajua kwamba watoto wengine wasiokuwa na wazazi huasiliwa na watu ambao hukusudia kuwachagua na kuwachukua kama wao. Ni heshima ilioje kuchaguliwa maksudi na wale ambao wanataka kumwaga upendo wao juu yao.

Hivi ndivyo haswa Mungu alivyotufanyia kama waaminio ndani ya Yesu. Kwa sababu ya kile ambacho Yesu alitufanyia msalabani, sasa tu wamojawapo wa familia yake milele, na Roho wake anakaa ndani yetu na hulia Aba, Baba. Baba Mungu aliamua kabla ya msingi wa ulimwengu kuwekwa kwamba, mtu yeyote atakayempenda Kristo atapendwa na kukubaliwa naye kama mwanawe. Aliamua atawaasili wote watakaomkubali Yesu kama mwokozi wao. Tunakuwa warithi wa Mungu na warithi pamoja na Mwanawe, Yesu Kristo.


Ni ufahamu wa uhusiano wetu wa kifamilia na Mungu ambao hutupatia ujasiri wa kwenda mbele ya kiti chake cha enzi na kufanya haja zetu zijulikane.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon