Roho wa Maombi

Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba… (ZEKARIA 12:10)

Kulingana na andiko la leo, Roho Mtakatifu ni Roho wa maombi, kumaanisha ni Roho wa maombi. Roho Mtakatifu hutupatia hamu ya kuomba; hiyo ndiyo moja ambayo huwa anatumia kutuzungumzia. Huenda tusigundue ni mara ngapi huwa anatuongoza kuomba na tukafikiria kwamba tuna mtu au hali fulani katika fikra zetu. Kujifunza kutambua Mungu anapotuambia tuombe huchukua muda mrefu na ni funzo ambalo kwa hakika nilijifunza kwa kufanya mazoezi.

Jumatatu moja, nilianza kufikiri juu ya mchungaji ninayemjua. Kwa muda wa siku tatu akaja katika fikra zangu bila kikomo. Jumatano nikamuona mhazigi wake nilipoenda kwa miadi mahali pa biashara na punde nikamuuliza alivyokuwa akiendelea. Niligundua kwamba mchungaji huyo alikuwa amekuwa mgonjwa wiki hiyo na, kuongezea, alikuwa ametambua kwamba baba yake alikuwa amegunduliwa kuwa ana saratani ambayo ilikuwa imeenea katika mwili wote.

Nikatambua mara moja kwa nini huyo mchungaji alikuwa moyoni mwangu sana wiki hiyo. Ni lazima nikiri sikuwa nimemwombea; nilikuwa tu nimemwaza. Bila shaka nilikuwa mwenye kujuta kuwa nilikosa uongozi wa Roho Mtakatifu, lakini nina hakika Mungu alitumia wengine kumwombea na kumhudumia nilipokuwa nikijifunza funzo hili muhimu kuhusu kusikia sauti yake.

Vitu kama hivyo vinapotufanyikia, hatufai kuhisi kuhukumika; tunafaa kujifunza tu. Roho wa maombi anaishi ndani yetu, hutuongoza, na kutuzungumzia. Tunahitaji kuendelea kukua katika uhisivu wetu kwa uongozi wake ili tuweze kuwaombea wengine anapotuambia kufanya hivyo na tutaona Mungu akifanya mambo makubwa katika maisha yao.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Ni bora kuombea mtu kuliko kuwaza kumhusu.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon