Shukrani Inayokuja na Neema

Shukrani Inayokuja na Neema

Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure. 1 Wakorintho 15:10

Iwapo mimi na wewe tutafikiri kwamba tunastahili kupokea tunachopokea kutoka kwa Mungu kwa sababu tumekichuma kwa matendo yetu mazuri—kiasi kikubwa cha maombi yetu, kusoma kwetu kwa Biblia kila siku, kutoa kwetu—basi hatutashukuru wala kuwa wenye shukrani. Kinyume na hilo, tutaanza kufikiri kwamba kila baraka tunayopokea ni ushahidi wa utakatifu wetu binafsi.

Lakini tunapoelewa kwamba kila baraka tunayopokea ni kwa sababu tu ya neema ya Mungu, na kamwe sio kwa sababu tunaistahili, mioyo yetu imebadilishwa. Tunajawa na shukrani kwa sababu ya wema wa Mungu. Hakuna kitu kinachoweza kutufanya tububujike na shukrani na sifa zaidi kuliko ufunuo wa neema ya Mungu ambayo imemiminwa bure juu ya maisha yetu.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru leo kwa wema wako katika maisha yangu. Ninajua kwamba sijafanya chochote kuustahili; unanibariki kwa kuwa unanipenda. Asante kwa upendo wako mtimilifu usio na masharti.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon