Tafuta Kile Kitu Kimoja

Tafuta Kile Kitu Kimoja

Neno moja nimelitaka kwa Bwana nalo ndilo nitakalolitafuta, nikae nyumbani mwa Bwana siku zote za maisha yangu, niutazame uzuri wa Bwana, na kutafakari hekaluni mwake. —ZABURI 27:4

Iwapo ungejua kwamba unataka tu kitu kimoja, ungeomba nini? Daudi alisema alikuwa tu na kitu kimoja ambacho alitafuta: kukaa nyumbani mwa Bwana.

Kuwa karibu na Mungu ndiyo kitu cha kwanza tunachofaa kuwa nacho maishani mwetu.

Lakini tunaweza kuwa na shughuli nyingi za maisha ya kila siku hadi tukapuuza kitu kilicho muhimu sana—kutumia muda wetu katika uwepo wa Mungu, tukimfurahia, kumjua na kutafuta uongozi wake.

Kuna watu wengi ulimwenguni wenye utupu katika maisha na hujaribu kuridhisha utupu ulio kwenye maisha yao kwa magari mapya, kupandishwa cheo, uhusiano, au kingine chochote kile. Lakini jitihada zao za kutafuta kutimizika kikamilifu katika vitu hivyo huwa hazifaulu, kwa sababu kila mmoja wetu ana utupu au shimo ambalo Mungu au utupu aliweka ndani yetu, na hakuna kinachoweza kulijaza isipokuwa Mungu Mwenyewe. Ninakuhimiza kumtafuta Mungu kwanza na uweke vile vitu vingine katika maisha yako baada yake. Ukimtanguliza katika kila kitu unachofanya, utabarikiwa kupita kiasi.


Mungu ndiye hicho “Kitu Kimoja” ambaye anaweza kukupa furaha kuu, amani, kuridhika na kutosheka.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon