Kuna fahari moja ya jua, na fahari nyingine ya mwezi, na fahari nyingine ya nyota; maana iko tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota. —1 WAKORINTHO 15:41
Sisi wote tuko tofauti. Kama jua, mwezi na nyota, Mungu ametuumba tukiwa tofauti, na amefanya hivyo kimaksudi. Kila mmoja wetu hutimiza hitaji fulani, na sisi sote ni sehemu mojawapo ya mpango jumla wa Mungu. Tunapojaribu kuwa kama mtu mwingine, tunapotea na kutoka kwenye yule mtu Mungu alituumba tuwe. Mungu alituumba tutoshe katika mpango wake, sio kuhisi tunasukumwa kujaribu kutoshea katika mpango wa kila mtu. Sio tu sawa kuwa tofauti bali ni vile ulivyoumbwa. Kila mmoja wetu huzaliwa na hali tofauti za moyo, maumbile tofauti, alama tofauti za vidole, vipawa na uwezo tofauti. Lengo letu linafaa kuwa kutambua kile ambacho tunapaswa kuwa binafsi, halafu tuwe na mafanikio katika kuwa kitu hicho. Ndiyo kwa sababu Warumi 12 inatufundisha kujipeana kwa vipawa vyetu. Tunafaa kutambua kile ambacho huwa tunakifanya vizuri halafu tujibwage ndani yake kwa moyo wetu wote.
Unaweza kuwa huru kupenda na kukubali wengine walio karibu nawe bila kuhisi msukumo wa kujilinganisha na kushindana nao. Watu waliotosheka, ambao wanajua Mungu anawapenda na ana mpango juu ya maisha yao huwa hawatishwi na uwezo wa watu wengine. Huwa wanafurahia kile watu wengine wanaweza kufanya, na hufurahia kile wanaweza kufanya pia.
Mungu alikupa vipawa na matamanio ile utumie. Lenga uwezo wako badala ya udhaifu wako.