Tunaweza Kuleta Utofauti

Na Bwana akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu wake (KUTOKA 32:14)

Je, unajua kwamba maombi hubadilisha mawazo ya Mungu? Kwa sababu ya mtu ambaye atachukua muda tu kuzungumza naye na kumsikiza, kwa kweli Mungu anaweza kubadilisha mawazo kuhusu alilokuwa amepanga kufanya.

Musa alipokwenda Mlima Sinai kuchukua amri kumi, alienda kwa muda mrefu kuliko vile watu walivyokuwa wametarajia. Bila kuwepo Musa, wakamsahau Bwana, wakatii tamaa za miili yao kwa kuamua kuyeyusha vito vyao na kutengeneza sanamu ya ndama, na kuiabudu. Mungu alizungumza na Musa mlimani akasema kimsingi, “Ni bora urudi kule chini kwa kuwa watu wamejinajisi. Na nimekasirika.” (Shukuru Mungu, Zaburi 30:5 inasema kwamba ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, na fadhili zake hudumu milele!)

Musa alianza kuwaombea watu kwa sababu aliwajali sana. Mungu alikuwa alikwishamwambia tayari, “Basi sasa niache, kwa kuwa hawa ni wenye shingo ngumu na wasumbufu” (soma Kutoka 32:9-10). Lakini Musa akakataa kusalimu amri kwa sababu jambo hilo lilimfadhaisha. Aliwapenda watu hao, alijua jinsi Mungu alivyokuwa na alijua sifa za Mungu. Isitoshe, alijua kwa kweli kwamba Mungu aliwapenda watu hao na hakutaka kuwaacha katika shida.

Musa akamwambia Mungu abadilishe mawazo yake (soma Kutoka 32:12) na kulingana na andiko la leo, Mungu alifanya hivyo. Tunaweza kuleta tofauti tunapoomba!

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Unapoomba, Mungu husikia na kujibu!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon