Uhusiano dhidi ya Dini

Uhusiano dhidi ya Dini

Kwa sababu hakuna mwenye mwili atahesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria. WARUMI 3:20

Yesu alikuwa na mengi ya kusema kuhusu dini, na haikuwa nzuri. Kwa nini? kwa sababu dini wakati wake ilikuwa na mara nyingi bado ni wazo la binadamu kuhusu kile Mungu anatarajia. Dini ni mtu kujaribu kumfikia Mungu kwa matendo yake mazuri.

Imani ya Mkristo inafundisha kwamba Mungu amemfikia binadamu kupitia kwa Yesu Kristo. Shukuru kuwa kwa kuweka imani yetu ndani ya Yesu, tunapokea faida ya kazi ambayo ametufanyia. Kazi yake—sio kazi yetu wenyewe, sio kufuata kaida na kanuni ambazo mwanadamu anaamuru—inatuhesabia haki kutufanya wasio na makosa kwake Mungu.

Mkristo sio tu mtu ambaye amekubali kufuata kaida na kanuni fulani na kuzingatia siku fulani kama takatifu. Mkristo ni mtu ambaye moyo wake umebadilishwa kwa imani ndani ya Yesu Kristo.


Sala ya Shukrani

Ninashukuru, Baba, kwamba niko huru kutokana na mawazo ya dini yaliyobuniwa na mwanadamu. Ninaweza kuhusiana nawe kwa njia ya kibinafsi, ya undani kwa sababu ya Yesu. Asante kwa kunipenda na kwa kuishi katika uhusiano nami.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon