Uhusiano Mzuri Sana Unaoweza Kuwa Nao

Uhusiano Mzuri Sana Unaoweza Kuwa Nao

Tazama nasimama mlangoni, nabisha, mtu akiisikia sauti yangu na kuufungua mlango nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. UFUNUO 3:20

Tuna haki kubwa ya kujenga uhusiano na Mungu na kumwalika kuwa sehemu muhimu ya kila kitu tunachofanya, kila siku. Hilo huanza kwa maombi rahisi—kuongea tu naye na kumwambia kuhusu maisha unapoendelea kufanya mambo yanayokupasa kufanya. Shukuru kwamba uwepo wako uko nawe, na umjumlishe katika fikra zako, katika mazungumzo yako, na katika shughuli zako zote za kila siku. Ukimtoa Mungu katika kisanduku cha Jumapili asubuhi ambacho watu wengi humueka, ukimruhusu kushambulia Jumatatu, Jumanne, Jumatano, Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi, na siku yote Jumapili pia, utashangaa tofauti itakayoleta. Usijaribu kumweka Mungu katika chumba cha dini; anataka uhuru wa kufikia kila eneo la maisha yako. Anataka kuhusika katika kila sehemu ya maisha yako. Anatamani uhusiano wa undani na wewe.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru Mungu kwamba unanipenda vya kutosha hata kutaka kuwa katika uhusiano nami. Ninataka kukugawia kila sehemu ya maisha yangu. Nisaidie kukumbuka kwamba uko nami kila dakika ya siku.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon