Ulinzi wa Bwana

Ulinzi wa Bwana

Aketiye mahali pa siri pake aliye juu atakaa katika uvuli wake Mwenyezi. —ZABURI 91:1

Uwepo wa Mungu ni mahali pa siri ambapo tunaweza kukaa kwa amani tukihisi salama, na kuingia rahani kwa Mungu. Hapa mahali pa siri si mahali panapoonekana; ni mahali pa kiroho ambapo wasiwasi huondoka na amani kutawala. Ni mahali pa uwepo wa Mungu. Tunapochukua muda kuomba na kumtafuta Mungu na kukaa katika uwepo wake, tuko katika mahali pa siri.

Tunapokaa ndani ya Yesu au katika mahali pa siri, hatutembelei tu mahali hapo mara moja moja bali tunapafanya kuwa makazi yetu ya kudumu. Ni mahali tunapokimbilia tunapodhurika, kuhangaika, au kuhisi unyonge. Ni mahali tunapokimbilia tunapotaabishwa au kuteswa, na tunapokuwa na hitaji kuu. Ni mahali pia ambapo huwa tunatolea shukrani na sifa kwa sababu ya wema wa Mungu katika maisha yetu. Ninapenda kusema uwepo wa Mungu ni mahali pangu pa kwanza pa kuenda ninapokuwa na hitaji lolote.

Ni muhimu tuwe tumepandwa kwa uthabiti ndani ya Mungu— kujua chanzo cha usaidizi wetu katika kila hali na kila mahali. Kwa usaidizi wa Mungu tunaweza kuwa na mahali petu binafsi pa siri na usalama kwa kumtegemea tu Mungu na kumtumainia kikamilifu. Hatujawahi kuwa zaidi ya wazo moja mbali na uwepo wa Mungu!


Mungu anataka tuwe na makazi chini ya ulinzi wa uvuli wa mabawa yake. Anataka tumkimbilie.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon