Una Uwezo

Una Uwezo

Tazama, nimewapa nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. —LUKA 10:19

Waamniyo wengi wamezimia, wadhaifu kwa kutoa uamuzi na kuugua kwa fikra za “siwezi.” Wanasumbuka kwa kukosa uwezo wa kiroho.

Mimi na wewe hatuna lazima ya kumrai Mungu kutupatia uwezo. Tunahitaji tu kutambua na kukubali kwamba tumepewa uwezo halafu tutembee kwa kile kilicho chetu tayari. Tunaweza kuanzisha na kudumisha “ufahamu wa uwezo”—fikra chokozi zilizojaa uwezo tele.

Mungu ametupatia uwezo wa kiroho kwa ajili ya vita vya kiroho. Uwezo wa kiroho huachiliwa imani yetu ikiwa thabiti. Tunapotembea ndani ya Mungu katika imani, tunaweza kukabili kila hali na fikra za kumshinda adui.

Fikra za matumaini zitatiririka kutoka kwetu tunapojua sisi ni nani ndani ya Kristo, jinsi anavyotaka kuwa karibu nasi, na uwezo ambao Biblia inasema ni wetu kupitia kwa imani.

Je, unatamani kuwa aaminiye mwenye uwezo mwingi? Jaribu kukabili kila hali katika maisha yako na imani nyepesi kama ya mtoto—ukiamini kwamba Mungu ni mwema, kwamba ana mpango mzuri juu ya maisha yako, na kwamba anashughulikia hali yako.


Una uwezo na Mamlaka ya jina la Yesu. Tembea katika nguvu za jina lake linaloshinda yote!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon