Unasikiliza?

Bwana akaja, akasimama, akaita vilevile kama kwanza, Samweli! Samweli! Ndipo Samweli akasema, nena Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikia (1 Samweli 3:10) 

Andiko la leo linatoka katika kisa ambacho Mungu alikuwa akitaka kumwambia Samweli alichokuwa akipanga kufanya  katika hali fulani. Ilimlazimu kuzungumza mara kadhaa kabla Samweli ajue kwamba sauti aliyosikia ilikuwa ya Mungu. Mara tu Samweli alipogundua Mungu alikuwa akizungumza naye, alijibu kwa kusema, “Ninasikiliza.”

Kusikia sauti ya Mungu ni muhimu kwa sababu ya kufurahia mipango yake juu ya maisha yako, lakini ikiwa utamsikiliza au ukose kumsikiliza ni uamuzi wa kibinafsi. Hakuna mtu mwingine yeyote anayeweza kukuamulia; lazima ujiamulie. Mungu anataka umsikilize. Hatakulazimisha kuchagua mapenzi yake, lakini atafanya lolote awezalo ili kukuhimiza kusema ndiyo kwake.

Mungu anataka ujue kile anachotaka ufanye, jinsi anavyohisi kukuhusu, na mipango yake juu ya maisha yako. Mithali 3:7 inasema “Usiwe mwenye hekima machoni pako.” Kwa maneno mengine, hata usifikirie kwamba unaweza kuendesha maisha yako na ukafanya kazi nzuri bila usaidizi na uelekezi wa Mungu. Kadri unavyokuwa na hakika kwamba unasikia sauti yake, ndivyo unavyopokea zaidi uelekezi na maagizo yake.

Amua leo kwamba Mungu anataka kuzungumza nawe, kwamba utasikiliza anapozungumza, na kwamba utaisikiliza sauti yake kikamilifu.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Mungu ana mipango mizuri juu ya maisha yako na atakuambia kila kitu unachohitaji kujua. Kumbuka kusikiliza!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon