Upaji Mwaminifu wa Mungu

Upaji Mwaminifu wa Mungu

Waangalieni ndege wa anagani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? MATHAYO 6:26

Mungu ni mwaminifu, na kwa sababu uaminifu umejikita katika tabia yake, hawezi kutupungukia wala kutusikitisha. Tajriba na Mungu hutupatia tajriba ya uaminifu wake. Sisi wote tuna mahitaji, lakini tunaweza kushukuru kwamba yeye hukidhi mahitaji hayo wakati wote. Huenda wakati wote asifanye kile tunachopenda, lakini yeye hufanya kitu sahihi. Huenda asije mapema lakini huwa hachelewi sana.

Nimeona Mungu akinitendea mara nyingi wakati wa miaka mingi ambayo nimekuwa nikimtumikia. Kwa kweli ninaweza kusema Mungu ni mwaminifu. Amenipa nguvu zinazohitajika, majibu ambayo yalikuja kwa wakati mzuri, marafiki wazuri katika mahali pazuri, milango ya nafasi iliyofunguka, himizo, fedha zilizohitajika, na mengine mengi. Na atakufanyia hivyo hivyo! Hakuna kitu tunachohitaji ambacho Mungu hawezi kutupa.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru leo, Baba, kwamba wewe ni mwaminifu. Upaji wako wakati wote huja vile ninavyouhitaji na huja haswa wakati ninaouhitaji. Nisaidie kukutazama wewe kwa upaji katika maisha yangu. Asante kwamba wewe ni zaidi ya kutosheka kwangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon