Ushindi Unastahili Gharama

Ushindi Unastahili Gharama

Maana kwa msaada wako nafuatia jeshi, kwa msaada wa Mungu wangu naruka ukuta. ZABURI 18:29

Katika Biblia yote, tunapata kwamba, amri za Mungu huja na ahadi ya thawabu wakati wote. Mungu sio mchukuaji; ni mpaji. Huwa hatuambii kufanya chochote isipokuwa ikiwa mwisho kitatufaidi.

Ninakuhakikishia: Vitu vyovyote ambavyo Mungu atawahi kukwambia ufanye, hata kama ni vigumu, hukwambia kwa kuwa ana kitu mawazoni kwa ajili yako—lakini ili uwe nacho, utahitaji kuchuchumilia mbele kwenye mahali pagumu.

Usiwaze au kusema, “Hii ni ngumu tu sana” unapojua kwamba unahitaji kufanya kitu. Shukuru kwamba Mungu hakuhitaji kujaribiwa kupita uwezavyo. Kwa kila tatizo, atafanya mlango wa kutokea. Huhitaji kusema, “Hakuna njia,” kwa sababu yeye ndiye njia (tazama Yohana 14:6) na hukufanyia njia. Unaweza kufanya chochote Mungu anakuita kufanya maishani! Una kile kinachohitajika ili ukifanye!


Sala ya Shukrani

Ninashukuru, Baba, hutaniambia nikabiliane na mambo nisiyoyaweza. Leo ninapochuchumilia mbele kupita kwenye sehemu zinazotatiza katika maisha yangu, ninakushukuru kwamba sichuchumilii mbele peke yangu—U nami!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon