Moyo Ulioridhika ni Moyo wenye Shukrani

Moyo Ulioridhika ni Moyo wenye Shukrani

Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa. 1TIMOTHEO 6:6 BIBLIA

Kuridhika na kuwa mwenye shukrani huenda pamoja. Watu ambao hawajaridhika hawajawahi kuwa na desturi ya kufurahia na kuwa wenye shukrani kwa baraka za kila siku katika maisha yao. Fikiria hili: ungekuwa hospitali sasa hivi, ungeridhika na kitu rahisi kama kukaa nyumbani kwako kwenye kiti chako ukipendacho, lakini ulipokuwa nyumbani katika kiti chako, pengine hukuridhika wakati huo pia. Mara nyingi huwa tunafikiria tutaridhika tutakapo…lakini kwa nini tusichague kuridhika sasa hivi?

Hata kama huna unachotaka au unachohitaji sasa hivi, kuwa na nia chanya na uwe mwenye wingi wa tumaini. Ridhika na kile ambacho Mungu amekupa, kataa kufikiri kuhusu kile usicho nacho, wapende wengine, na ukae ukiwa na matumaini kuhusu kila eneo la maisha yako.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru, Mungu, kwamba umenipa baraka nyingi za kila siku. Nisaidie kuridhika na nisiidharau hata moja. Hata ninapokungoja kwa ajili ya vitu ambavyo ninaomba kwavyo, ninachagua kuwa mwenye shukrani kwa baraka ninazoishi ndani yake kila siku.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon