Wewe si Mshinde

Wewe si Mshinde

Akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo. —WAKOLOSAI 2:15

Watu ambao wameteswa, kukataliwa au kutekelezwa hukosa ujasiri mara nyingi. Watu kama hao huona aibu, huhukumika na kuwa na picha mbaya kujihusu. Shetani hujua hilo na kuanza kushambulia ujasiri wao wa kibinafsi wakati wowote na mahali popote anapopata mpenyo. Lengo lake huwa kufanya watu waamini ni washinde.

Shetani anajua kwamba, mtu asiye na ujasiri hawezi kuchukua hatua ya kufanya mambo ambayo kwa kweli wanataka kufanya. Hataki utimize mapenzi ya Mungu juu ya maisha yako. Iwapo ataweza kukufanya uamini kwamba huwezi, basi hutajaribu hata kukamilisha kitu cha maana. Hata kama utafanya bidii, hofu yako ya kushindwa itaupiga muhuri ushinde wako, ambao kwa sababu ya kukosa ujasiri, bila shaka uliutarajia tangu mwanzo. Hii mara nyingi hujulikana kama “Dalili ya Ushinde.” Watu hukosa kufanikiwa kwa sababu ya imani mbaya, na wanaendelea kuwa imani mbaya kwa sababu ya kutofaulu. Ni vigumu ni ipi hutangulia, lakini hujipata katika mtego ambao haonekani kujinasua.

Yesu alimshinda Shetani na kumshangilia katika msalaba, na ushindi wake ni wetu. Unaweza kushinda dalili ya ushinde kwa sababu wewe ni zaidi ya mshindi kupitia kwa Kristo (Warumi 8:37).

Ushindi wa Mungu ulionunuliwa msalabani ni mkamilifu na mtimilifu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon