Kujitunza

Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe, maana mlinunuliwa kwa thamani, sasa basi mtukuzeni Mungu katika miili yenu. —1 WAKORINTHO 6:19–20

Mungu huita kila mmoja wetu kufanya kitu maalumu katika maisha haya. Lakini ili kufanya hivyo, ni muhimu kuamua kutunza mwili wetu—nyumba aliyotupatia kuishi ndani yake. Ili kutimiza kusudi alililotupatia Mungu, tunaweza kuchagua kutafuta kiasi katika kile tunachokula na kunywa, kupata kupumzika vizuri na kufanya mazoezi, na kudumisha mtindo wa maisha wenye afya.

Hakuna kitu kibaya kama kupitia katika maisha ukihisi vibaya kila wakati. Kama mtu aliyeng’ang’ana na uteuzi wa lishe na wasiwasi ya uzani kwa miaka mingi, ninajua hisia vizuri sana. Tunapokuwa hatuna afya na kukosa kiasi, huwa hatuhisi tu vizuri. Ni vigumu kufanya kile Mungu ametuita kufanya miili yetu ikiwa ni ya kujivuta kwa sababu hatujaitunza kwa njia inayofaa.

Ninaamini kwamba ni jambo la kiroho kuujua mwili wako, unachohitaji, na kile ambacho kinaufaa. Ukiishi katika uhusiano wa karibu na Mungu, maisha yako yote yanaathiriwa—roho, nafsi na mwili. Ninakuhimiza leo kumwomba Mungu akusaidie kuamua kufanya uteuzi mzuri wa busara ambao utafaidi mwili aliokupa.


Mwombe Mungu akusaidie kufuata uongozi chanya wenye afya wa Roho Mtakatifu na kukataa vichocheo hasi vya mwili.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon