Kushinda Picha Mbaya ya Vile Unavyojiona

Kushinda Picha Mbaya ya Vile Unavyojiona

Mungu akasema, na tumfanye [Baba, Mwana na Roho Mtakatifu] mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu… —Mwanzo 1:26

2 Samweli sura ya tisa inaeleza kisa cha Mefiboshethi, mjukuu wa Mfalme Sauli na mwanawe Yonathani. Akiwa mlemavu kama kijana, Mefiboshethi alijiona kama mtu asiyefaa. Badala ya kujiona kama mrithi wa haki wa urithi wa babake na babu yake, alijiona kama mtu ambaye angekataliwa.

Daudi alipotumana Mefiboshethi kufikishwa kwake, alianguka kifudifudi mbele ya mfalme na kuonyesha hofu. Daudi akamwambia asiogope, kwamba alikusudia kumtendea Mefiboshethi mema kwa sababu ya agano lake na Yonathani. Jibu la kwanza la Mefiboshethi ni mfano muhimu wa aina mbaya ya picha ya vile tunavyojiona ambao sisi sote tunahitaji kushinda.

Picha mbaya ya vile tunavyojiona hutusababisha kutembea katika hofu badala ya imani. Tunatazama makosa tuliyofanya badala ya mambo mazuri ambayo Yesu amefanya. Amechukua dhambi zetu na kutupatia haki yake (2 Wakorintho 5:21). Tunaweza kutembea kwa furaha katika uhalisia wa ukweli huo.

Ninapenda mwisho wa kisa hicho. Daudi alimbariki Mefiboshethi kwa ajili ya Yonathani. Alimpa wahudumu na ardhi na kukimu mahitaji yake yote. Mungu atatubariki kwa ajili ya Yesu!

Sisi sote twaweza kuhusisha ulemavu wa Mefiboshethi na udhaifu wetu. Tunaweza pia kuwa na ushirika na kula na Mfalme wetu Yesu—bila kujali makosa na udhaifu wetu.


Tuna agano na Mungu, iliyofungika na kuidhinishwa katika damu ya Yesu Kristo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon