Uhuru Kutokana na Kujihurumia

Uhuru Kutokana na Kujihurumia

Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi kutembea kwa muda wa miaka thelathini na minane. Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, “Wataka kuwa mzima?” (Kweli una hakika unataka kupona?) —Yohana 5:5– 6

Kwa miaka mingi sana, “Kwa nini mimi, Mungu?” Kilikuwa kilio cha moyo wangu, na kilijaza mawazo yangu na kuathiri fikra zangu kila siku. Niliishi katika jangwa la kujihurumia, na likawa tatizo kwangu, familia yangu, na mpango wa Mungu juu ya maisha yangu. Nilihisi kana kwamba nilihitaji kulipwa kutokana na vile niliteswa nikiwa mtoto, lakini nilikuwa nikitarajia watu kunilipa wakati ningekuwa ninamtazama Mungu.

Yesu alipokutana na mwanamume aliyekuwa amelala kando ya birika ya Bethzatha kwa muda wa miaka thelathini akingoja muujiza, alimwuliza iwapo kweli alikuwa akitaka kupona. Watu wengi wangependa kupata muujiza, lakini kama mwanamume wa kisa chetu, hawako tayari kuacha kujihurumia na kujilaumu.

Mungu anataka kutupatia urembo mahali pa jivu, lakini lazima tuwe tayari kuachilia jivu! Hiyo inamaanisha, kuacha kujihurumia, kujilaumu, na kuwa na fikra za uchungu. Siku hizi unaweza kuwa mwanzo mpya kwa mtu yeyote aliye tayari kusahau yaliyopita na kumfuata Yesu kikweli!


Tunaweza kuwa wenye kujihurumia sana au wenye nguvu, lakini hatuwezi kuwa vyote. Chagua kuacha kujihurumia ili kuwa huru.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon