Aina Nzuri ya Mzigo

Walakini uyaelekee maombi ya mtumwa wako, na dua yake, Ee Bwana Mungu wangu, uisikilize sauti na maombi ya mtumwa wako, aombayo mbele zako leo (1 WAFALME 8:28)

Wakati mwingine unapowaombea wengine, utapita kila wengine huita mzigo wa maombi au mzigo wa uombezi. Mzigo ni kitu kinachokuja moyoni mwako na kukihisi kwamba ni kizito na muhimu; ni kitu ambacho Mungu anatuambia tubebe katika maombi; ni kitu usichoweza kukung’uta. Huenda wakati mwingine Mungu akakuzungumzia na kukueleza kuhusu huo mzigo. Wakati mwingine huwezi kujua mzigo huo unahusu nini au huelewi kikamilifu, unajua tu kwamba lazima uombe.

Watu wengine huitwa kuombea vitu fulani sana. Mume wangu anaiombea Marekani sana. Ninajua watu wanaoiombea Israeli kila wakati. Mwanamke mmoja aliniambia aliombea wakongwe waliokuwa wanarejea kutoka vitani. Ninaamini Mungu anashughulikia kila hitaji ulimwenguni. Sisi sote hatuhitaji kuombea kitu kimoja kwa sababu tukifanya hivyo, mahitaji yote hayatashughulikiwa. Sikiliza kile ambacho Mungu ameweka katika moyo wako na ukiombee.

Njia mojawapo ambayo Mungu huzungumza nasi ni kupitia kutupatia mizigo ya wengine. Hufanya hivi mara nyingi bila kuzungumza lakini kwa hisia za uzito na kujali watu katika mioyo yetu. Hili linapofanyika, anatuambia tuwaombee. Sikiliza anakupa mizigo gani na uwe mwaminifu kuomba anapokuambia ufanye hivyo.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Unapoombea wengine, kumbuka kwamba Mungu pia ana mtu anayekuombea.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon