Chanzo cha Imani Yako

Chanzo cha Imani Yako

Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. WAFILIPI 4:13

Tunapokuwa na imani ndani ya Mungu na kuchagua kuwa salama ndani yake, tunaweza kupiga hatua ya kuishi kwa imani na kufurahia maisha ambayo anataka kwa ajili yetu. Kumbuka nimesema kwamba “imani ndani ya Mungu,” sio ndani yetu. Mara nyingi watu wanapofikiri kuhusu imani, wanafikiri kuhusu kujiamini. Kuna sauti nyingi katika jamii zinazokusihi “kujiamini!” Hicho ndicho kitu tusichotaka kufanya! Lazima imani yetu iwe ndani ya Kristo peke yake sio ndani yetu, sio ndani ya watu wengine, sio katika ulimwengu au mifumo yake.

Shukuru kuwa tunaweza kuwa na imani iliyo na mizizi yake katika Kristo, tukijua kuwa Yeye ni kila kitu tunachohitaji—Yeye ni zaidi ya vyote! Biblia inaeleza kwamba sisi ni watoshelevu katika utoshelevu wa Kristo (tazama Wafilipi 4:13). Njia nyingine ya kuisema itakuwa, “tuna imani tu kwa sababu anaishi ndani yetu, tunapata nguvu kutokana na imani Yake.” Kwa hivyo nenda uishi kwa imani leo—imani ndani ya Kristo na uwepo wake katika maisha yako.


Sala ya Shukrani

Ninashukuru, Baba, kwamba sina haja ya kupitia maishani bila usalama na upungufu wa imani. Kwa sababu ya uwepo wako na nguvu katika maisha yangu, ninaweza kuwa na ujasiri mpya na furaha ambayo sijawahi kuwa nayo. Asante kwa nguvu zako ambazo huniwezesha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon