Je, Inastahili?

Je, Inastahili?

. . . Kwa hivyo amani, upendo na amani. —ZEKARIA 8:19 NKJV

Ni matamanio ya Mungu ya kweli kwako wewe kuishi maisha ya yaliyojaa amani. Kadri unavyomkaribia—ndivyo utakavyopata amani zaidi.

Hakuna nafasi au mali iliyo na maana iwapo huna amani. Hela, umaarufu, hadhi—vyote havina maana iwapo huna amani. Huwezi kupiga bei ya thamani ya amani.

Watu wengi hutumia maisha yao wakijaribu kupanda ngazi ya mafanikio, lakini kila wakati wanapopanda ngazi moja kuelekea juu, wanapoteza amani yao zaidi pamoja na furaha na wakati wa kuwa na familia zao. Maisha yao yote yanaharibiwa na mshinikizo na mfadhaiko wa kujaribu kulinda walivyopata. Lakini hatuwezi kuwa tumefanikiwa kwa kweli kama hatuna amani.

Wengine wanafanya kazi nyingi ili kupata kile ambacho ulimwengu unaning’iniza machoni mwao, ukisema, “lazima uwe na hiki kwa kweli uwe na furaha.” Wanapata “vitu,” hivyo lakini bado hawana amani yoyote.

Warumi 14:17 inatuambia, “Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa”—sio vitu ambavyo hela au hadhi inaweza kupeana —lakini ni “haki, na amani, na furaha ndani ya Roho Mtakatifu.” Ufalme wa Mungu unapatikana kutokana na kujua sisi ni akina nani ndani ya Yesu na kuwa na “amani ya Mungu, ipitayo ufahamu wote” (Wafilipi, 4:7).


Mungu anataka mahitaji yako yatimizwe kwa wingi na uwe katika nafasi ya kubariki wengine. Usitie shaka kwamba Mungu antaka kukubariki, lakini usitafute kuwa na chochote kama huwezi kuwa nacho kwa amani.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon