Kuchagua Vita Vyako

Kuchagua Vita Vyako

Sasa Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote. 2 Wathesalonike 3:16

Ninaamini mojawapo ya njia nzuri za kufurahia wakati uliopo na kuepuka mfadhaiko usiokuwa na maana ni kukataa kuacha kila kitu kidogo kukukasirisha. Kwa maneno mengine, chagua vita vyako, na usifanye jambo dogo kuwa kubwa.

Kabla ya kutenga wakati, nguvu, na hisia kwa ajili ya hali au jambo fulani, jiulize maswali mawili. Kwanza, jiulize iwapo lina umuhimu wowote; pili, jiulize kama wakati, jitihada na nguvu utakazotia hapo zinafaa kweli kutiwa hapo.

Kwa kweli jua kilicho muhimu katika maisha, shukuru kwa vitu hivi na uvitafakari. Jifunze kutambua tofauti kati ya mambo makubwa na mambo madogo. Bila kuongeza mambo mengine, maisha yamejaa mapambano. Unapojaribiwa kuanzisha mradi, sita kwanza na ufanye uamuzi iwapo utastahili utakayoyahitaji kutoka kwako.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba unanipa hekima ya kutambua kati ya vitu ambavyo ni muhimu na visivyo muhimu. Ninaomba kwamba utanisaidia kujifunza kuachana na vitu visivyo muhimu. Asante kwa kuwa ninaweza kuokoa wakati na nguvu kwa ajili ya vitu ambavyo kwa kweli ni vya muhimu

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon