kufanya maamuzi magumu

kufanya maamuzi magumu

Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Waebrania 4:15

 Ni muhimu kufanya uchaguzi sahihi, hasa wakati wa kuumiza, kukata tamaa, kugandamizwa na kuchanganyikiwa – wakati uchaguzi sahihi ni uchaguzi mgumu kufanya. Wakati vitu vinatusonga, kwa kawaida tunapenda kuchukua njia ya upinzani mdogo. Lakini hizo ni nyakati fupi wakati kufanya uchaguzi sahihi kunaweza kufanya tofauti kubwa zaidi.

Kwa sababu ya kuvuna matokeo mazuri katika maisha, unapaswa kufanya haki wakati hauhisi kufanya hivyo. Kinachonishangaza ni kwamba Yesu anajua tunavyojisikia. Alipokuwa mwanadamu, alikumbana na matatizo yote tunayopambana nao. Alihisi kama kuacha na kuchukua njia rahisi, lakini alishinda na kufanya uchaguzi mgumu.

Tunapokuwa na uchovu na kukata tamaa katika uamuzi wetu, tunaweza kujua kwa ujasiri kwamba tunamtumikia Mungu ambaye anajua kile tunachopitia. Anataka kutusaidia na kutupa neema Yake kwa hiyo hatuna haja kufanya maamuzi magumu wenyewe.

Unapojikuta umechoka au karibu kukata tamaa, kumbuka kwamba Mungu yu pamoja nawe na anaelewa. Pata nguvu kufanya uchaguzi mgumu ndani yake.

 OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, nimefurahi sana na ninashukuru kwamba unaelewa kila kitu ninachokipitia na kukabiliana nacho. Ninapojaribiwa kuchukua njia ya upinzani mdogo, nitapata nguvu zangu ndani yako kufanya uchaguzi mgumu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon