Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. WAEFESO 4:15
Mungu hatutarajii kuwa watimilifu. Kwa kweli ni sahihi kabisa kwa sababu hatungekuwa watimilifu ndipo akamtuma Yesu kutuokoa na Roho Mtakatifu kutusaidia katika maisha yetu ya kila siku. Iwapo tungeweza kufanya hivyo binafsi, tusingehitaji usaidizi. Shukuru kwamba Yesu alikuja kusamehe makosa yetu na kuyafuta machoni mwa Mungu. Kwa kweli sisi ni watimilifu kupitia kwa Yesu, lakini hatuwezi kuwa watimilifu katika matendo yetu binafsi.
Yesu alisema, “Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu” (Mathayo 5:48), lakini uchunguzi wa lugha asilia unaonyesha kwamba alimaanisha tunafaa kukua hadi kwenye ukomavu wa nia na tabia ya kiungu. Mungu hajasikitika kuwa hatujafikia kudhihirisha tabia timilifu, lakini hupendezwa kutupata tukikua hadi kwenye ukomavu.
Sala ya Shukrani
Baba, ninashukuru kwamba unanisaidia kukua hadi kwenye ukamilifu wa kiroho na ukomavu. Sijatimilika, lakini kwa sababu ya kazi yako, ninakushukuru kwamba niko sawa na niko njiani!