Kukubali Mtu Mungu Alikuumba Kuwa

. . . Na aache mabaya, atende mema; atafute amani, aifuate sana. (Usitamani tu uhusiano wa amani kati yako na Mungu, wanadamu wenzako, na wewe mwenyewe binafsi, lakini ifuate!] —Waraka Wa 1 Petro 3:11 (Msisitizo Umeongezwa)

Katika miaka yangu ya huduma, nimegundua watu wengi hawajipendi kweli. Hujikataa! Hili ni tatizo kubwa zaidi kuliko vile tunavyofikiri. Bila shaka sio mapenzi ya Mungu kwa watoto wake kuwa kinyume na wao binafsi. Kabisa, ni sehemu ya mpango wa shetani kujaribu kutufanya tutaabike na kutuzuia kupenda watu.

Iwapo hatutajikubali, hatutawakubali watu wengine. Tukikataa, tutaanza kufikiria watu wametukataa pia. Mahusiano ni sehemu muhimu ya maisha yetu. Jinsi tunavyohisi kujihusu ni jambo linaloamua mafanikio yetu katika maisha na katika mahusiano. Tunahitaji kumwamini Yesu kabisa!

Picha yetu binafsi ya vile tunavyoonekana ni picha yetu ya mtu wa ndani tuliyo nayo kujihusu. Iwapo tunachoona si kizuri na si ukweli kulingana na Maandiko, tutataabika kutokana na hofu, kukosa usalama, na mawazo mengine potovu kutuhusu.

Mungu anatupenda na anataka tukubali upendo wake. Na kwa sababu ya upendo wake, tunaweza kujipenda kwa njia nzuri iliyo na kiasi. Sisi ni watoto wa Mungu—watu wanaopendwa, kukubaliwa, na kwa neema yake tunaboreka kila siku!


Yesu alikuja kuleta urejesho katika maisha yetu. Mojawapo ya vitu alivyokuja kurejesha ni picha yetu binafsi nzuri iliyo na kiasi.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon