Kumkaribia Mungu Kila Siku

Kumkaribia Mungu Kila Siku

Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho. —YOHANA 6:40

Maisha ya Mkristo hayakukusudiwa kuwa ya kufuata kanuni na kutimiza orodha ya mahitaji. Ndiyo, Mungu hutupa miongozo na maagizo ya kuishi, lakini haya hayakusudiwi kuwa wajibu wa kidini; ni kanuni zitakazotusaidia kutambua maisha tele yaliyojaa furaha na yanayofurika ambayo Yesu alikufa kutupatia.

Mungu anatamani ukiuke mipaka ya “dini” na uishi katika uhusiano wa ndani tena wa karibu sana naye. Hivi ndivyo inavyomaanisha kumkaribia Mungu. Sio Mungu wa mbali wa kisheria, asiyejali na asiyefikika. Mungu ni Baba yako wa mbinguni ambaye anakupenda bila masharti na asiyekosa kukupenda.

Haijalishi ya kale, hata kama umekosea mara ngapi, haijalishi kasoro unazofikiri kwamba unazo, unaweza kuishi katika uhusiano wa karibu na Mungu. Atakufariji. Atatembea nawe. Na hatakupungukia wala kukuacha kabisa.

Mungu anakupenda zaidi ya vile ungeweza kufikiri. Kile unachofaa kufanya ni kupokea upendo wake.


Kuishi “karibu na Mungu kila siku” ni kupokea upendo wa Mungu na kujifunza kumpenda pia.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon