Kumwandama Mungu

Kumwandama Mungu

Nafsi yangu inakuandama sana; mkono wako wa kuume unanitegemeza. —ZABURI 63:8

Ninakumbuka utupu niliohisi miaka mingi iliyopita nilipogundua kwamba wakati mwingine nilikuwa na furaha ya muda lakini siyo ya ndani inayoridhisha. Uhusiano wangu na Mungu ulikuwa kama wa Waisraeli ambao wangemwona tu Mungu kwa mbali huku Musa akizungumza na Mungu ana kwa ana. Nilitaka kutembea karibu zaidi na Mungu, lakini sikujua vile ningefanya hivyo

Pengine unapitia niliyoyapitia. Niliishi kwa sheria, nikifanya mambo ambayo kanisa langu lilifunza, nikitarajia desturi ya kazi zangu nzuri kuleta amani, furaha na nguvu za kiroho ambazo Maandiko yanaahidi. Badala yake nilijipata nikiwa nimevunjika moyo sana kiasi kwamba hakuna kilichokuwa kikifanya kazi. Hadi nilipojifunza kuacha “kujaribu kufanyia” Mungu mengi na kuwa tu katika uhusiano naye ndipo nilianza kuishi kwa amani na kuridhika kutoka kwa Bwana.

Ukitaka baraka na nguvu za Mungu, kuwa na hamu na umwandame. Weka kando vitu vingine na umfuatilie. Fanya yale Daudi alisema kuhusu katika Zaburi 27:4 kwamba jitoe kwa kitu kimoja—uwepo unaodhihirika wa Mungu.

Kitu cha pekee ambacho kwa kweli huridhisha hamu ya ndani ni kumjua Mungu kwa undani leo kuliko tulivyomjua jana.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon