Kusherehekea Maisha, Kusherehekea Mungu

Kusherehekea Maisha, Kusherehekea Mungu

Nao walikuwa daima ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu. LUKA 24:53

Jaribu kuanza kila siku kwa kusema, “Ninapenda maisha yangu!” Maneno yetu wenyewe huathiri hali yetu ya moyo, kwa hivyo ni vizuri kusema kitu ambacho kitakusidia kuhisi vizuri badala ya kitu ambacho kitakufanya ukasirike. Unaweza kufanya kushinda ukiwa na furaha kuwe kama mchezo unaoburudisha. Chunguza siku ambazo unaweza kukaa bila kuwa kwenye hali mbaya ya moyo au kulalamika.

Kusherehekea maisha ni kitu tunachofaa kufanya kimaksudi kwa sababu tunafahamu uzima ulivyo kipaji cha ajabu. Mungu ni uzima (tazama Yohana 1:4), kwa hivyo kwa kweli, tunaposherehekea uzima, tunamsherehekea Mungu. Bila yeye kusingekuwa na uzima kamwe. Jaribu kuunda hali bora ya moyo kwa kusema, “Ninashukuru na ninapenda uzima!” Iwapo kweli unataka kuhisi vizuri, jaribu hili: “Ninampenda Mungu, ninayapenda maisha yangu, ninajipenda, na ninawapenda watu.”


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwamba mimi si mfungwa wa hali ya moyo wangu. Ninaweza kuongea maneno chanya yaliyojaa imani na kuboresha nia yangu na siku yangu. Ninashukuru kwa maisha uliyonipa, Baba, ninayapenda maisha yangu!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon