Kushikilia Kwa Kuongozwa na Roho

Imekuwaje basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; mtaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia (1WAKORINTHO 14:15) 

Kwa kweli ninataka kukuhimiza kuomba maombi ya kushikilia na yenye subira kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu- sio maombi matupu ya kujirudiarudia ambayo hayatoki moyoni mwako, lakini maombi yanayokataa kusalimu amri. Inawezekana kutumia mdomo wako kuzungumza maneno ya maombi ambayo hayana maana kabisa ndani yake, na maombi hayo si kitu ila kazi iliyokufa. Ninaweza kunukuu sala yote ya Bwana huku nikiwa ninawaza kuhusu kitu kingine, na haitambariki Mungu au kunitenda wema, lakini nikiwa mwaminifu na kuomba kutoka moyoni mwangu, Mungu husikia na kufanya kazi kwa niaba yangu.

Huduma ya midomo haimfanyii Mungu chochote au kukamilisha chochote katika maisha yetu, kwa hivyo hata tunapoomba, kuhusu kitu hicho hicho tena na tena, tunahitaji kuwa waangalifu tusije tukajipata tukifanya marudio yasiyo ya maana. Badala yake, tunahitaji kumruhusu Roho Mtakatifu kutuongoza kwa njia mpya, hata kama tunashughulikia jambo ambalo tumeombea kwa muda mrefu. Wakati mwingine atatuongoza kuwa na bidii na kushikilia jambo, lakini kuna tofauti kati ya kujirudia na kushikilia kwa kuongozwa na Roho.

Maneno yaliyosemwa katika maombi bila kutoka mioyoni mwetu ni maneno yasiyo na nguvu. Tunapoomba tunafaa kutazama na kuwa wamakinifu kwa kile tunachosema. Hatufai tu kuzungumza kwa sauti kile ambacho tumeweka mioyoni mwetu huku mioyo hiyo ikiwa mbali na Mungu. Maombi ya bidii (kutoka moyoni, ya kuendelea) ya mwenye haki huachilia nguvu kuu ipatikane (soma Yakobo 5:16).

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Maombi yanayotoka moyoni huwa na nguvu na Mungu huyasikia.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon