Kusikiliza Sauti Yake

Kusikiliza Sauti Yake

Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. Warumi 10:17 Biblia

Kujifunza kusikia kutoka kwa Mungu husisimua sana. Mungu anataka kuongea nasi kuhusu mpango alio nao kwa ajili ya maisha yetu. Mpango wake ni mzuri, lakini tuko katika hatari ya kuukosa iwapo hatutajifunza kuisikiza na kuitii sauti ya Mungu.

Mungu husema nasi kwa njia nyingi sana. Husema nasi kupitia kwa Roho Mtakatifu wake anayeishi ndani yetu, kupitia kwa “kujua” iliyo ndani kabisa, na kupitia kwa amani. Huenda pia akaongea kupitia kwa watu wengine, hali, hekima, mazingira, na hata kupitia kwa ndoto na maono.

Hata hivyo, njia ambazo Mungu husema nasi sana ni kupitia kwa Neno lake na mshahidi wa ndani katika mioyo yetu. Neno la Mungu ni kipawa cha thamani ambacho tunafaa kushukuru kwacho kwa sababu ni ujumbe wa moja kwa moja kutoka kwa Mungu hadi kwetu sisi—ni Neno lisilobadilika na lisiloshindwa. Unapojifunza kusikia kutoka kwa Mungu, hakikisha wakati wote kwamba, ushahidi wa ndani wa moyo wako unalingana na Andiko.


Sala ya Shukrani

Baba, asante, kwamba bado ungali unaongea na wanao. Ninaomba unisaidie kukusikia na kufuata mwelekeo wako kwa ajili ya maisha yangu. Asante kwa kuwa unanifunza jinsi ya kufuata uongozi wako katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon