Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri [yanayostahili kutamaniwa], lakini mti mwovu [unaooza, usio na thamani] huzaa matunda mabaya [yasiyo na thamani]. —MATHAYO MTAKATIFU 7:17
Tunda lililo katika maisha yetu (tabia zetu) hutoka mahali. Mtu mwenye hasira yuko vile kwa sababu fulani. Majibu yake ni tunda baya la mti mbaya ulio na mashina mabaya. Ni muhimu kwetu sisi kuchunguza kwa uaminifu tunda letu pamoja na mashina yetu.
Katika maisha yangu binafsi, kulikuwa na matunda mengi mabaya. Nilishikwa na mifadhaiko ya ghafla mara kwa mara, mawazo hasi, kujihurumia, hasira za haraka, na mwenye kujiona bora kuliko ilivyostahili. Nilikuwa mkali, nisiyebadilika, mzingatia sheria, na mwenye kuhukumu. Nilishika kinyongo na nilikuwa mwoga.
Nilitia bidii katika kurekebisha hali hii. Ilhali ilionekana kwamba kadri nilivyojaribu kujiepusha na tabia mbaya, mbili au tatu zingetokea ghafla kama magugu. Sikuwa nafikia shina lililofichika la tatizo na hivyo halingekufa.
Iwapo hali hii inasikika kuwa ya mazoea kwako, huenda ikawa una mambo ambayo hujatatua katika maisha yako ambayo yanahitaji kusakwa na kuondolewa ili kila kitu kianzwe upya. Usitoroke. Kama Mungu anaweza kunibadilisha, bila shaka anaweza kukubadilisha.
Tunda lililooza hutoka kwa mashina yaliooza; tunda zuri hutoka kwa mashina mazuri.