Maisha Yanayompendeza Mungu

Maisha Yanayompendeza Mungu

Basi wapenzi wangu kwa kuwa tuna ahadi hizo na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu. —2 WAKORINTHO 7:1

Ili kuishi katika uhusiano wa karibu na Mungu, kuna maamuzi mengine ambayo tunafaa kufanya kila siku. Kuna nyakati ambazo tutahitaji kukataa vitu vingine ambayo tungevikubali na kukubali vitu vingine ambavyo tungekataa. Hili huhitaji hekima na ujidhibiti wa kibinafsi, lakini kwa shukrani, Roho Mtakatifu hutupatia hivi vyote.

Ni muhimu kufundisha watu kuishi maisha ya matakatifu kwa sababu ni sehemu muhimu ya kuishi katika uhusiano wa karibu na Mungu. Haimaanishi kwamba hatutawahi kufanya makosa—inamaanisha tu kwamba matamanio ya mioyo yetu ni kuishi kwa namna ambayo inampendeza Bwana. Hili linatimizwa kwa kutafuta kupendeza Mungu katika mawazo, mazungumzo, ushirika, muziki, burudani na mengineyo.

Iwapo mwili wetu unatamani kwenda njia nyingine lakini Neno la Mungu la Mungu linatufundisha kwenda njia nyingine, tunaweza kupokea neema ya Mungu ili kutii anachosema. Habari njema ni kwamba kuna thawabu kubwa tunapofanya hivyo.

Tunapochagua kumwishia Mungu maisha yetu, badala ya yetu binafsi, tutafurahia haki, amani, na furaha ndani ya Roho Mtakatifu. Tutaishi katika ushindi bila kujali kinachotukabili. Hayo ni maisha mazuri—hayo ndiyo maisha teletele, ya ushindi, yaliyojaa furaha ambayo Yesu alikufa kutupatia.


Wekeza katika mustakabali wako: Chagua kuishi maisha ya kutochanganya kwa ajili ya Mungu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon