Maombi ya Bidii Kweli

Maombi ya Bidii Kweli

. . . Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. —YAKOBO 5:16

Iwapo umekuwa aaminiye kwa kipindi chochote cha muda, bila shaka umesikia ikifunzwa kwamba ili maombi yawe yenye mafanikio, lazima yafanywe kwa bidii. Hata hivyo tukikosa kuelewa neno bidii, huenda tutafikiri kwamba lazima tuchochee hisia zenye nguvu kabla hatujaomba; la sivyo maombi yetu hayatakuwa yenye mafanikio.

Ninajua kuna miaka mingi ambayo niliamini hivyo, na pengine pia wewe umefundishwa vibaya hivyo. Lakini kuomba kwa bidii humaanisha tu kwamba lazima maombi yetu yatoke moyoni na yawe ya kweli.

Ninakumbuka nikifurahia nyakati za maombi nilipokuwa nikihisi uwezo wa Mungu, na kuanza kushangaa ni kitu gani kilikuwa kibaya wakati ambao sikuwa ninahisi chochote. Baada ya muda nikajifunza kwamba imani haikutegemea hisia au hisi lakini maarifa yaliyo moyo.

Wakati mwingine huwa na kuwa na hisia kuu ninapoomba. Lakini kuna nyakati nyingi ambazo huwa sihisi hisia. Maombi yanayotuleta karibu na Mungu hufanyika tu tunapoomba kwa imani, bila kujali tunavyohisi wakati fulani wowote.


Tumaini kwamba maombi yako ya dhati na bidii yana mafanikio kwa sababu imani yako iko ndani ya Mungu, sio katika uwezo wako mwenyewe wa kuomba kwa shauku au ufasaha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon