Mfano Wa Kristo

Mfano wa Kristo

Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. —Warumi 8:29

Lengo zuri sana ambalo Mkristo anaweza kuwa nalo ni kufanana na Yesu. Yesu ni mfano wa moja kwa moja wa Baba, na tumeitwa kufuata nyayo zake. Alikuja kama mwanzilishi wa imani yetu kutuonyesha kwa mfano vile tunavyoweza kuishi. Tuna nafasi ya kuwa na tabia ambazo Yesu alikuwa nazo miongoni mwa watu. Lengo letu sio kuona vile tutakavyofanikiwa katika biashara au vile tutakavyokuwa watajika. Si mali, umaarufu, au hata kujenga huduma kubwa, lakini kubadilishwa hadi tuwe mfano wa Yesu Kristo.

Ukomavu wa kiroho au mfano wa Yesu hauwezi kupatikana bila “nafsi kufa.” Hiyo inamaanisha, kusema ndiyo kwa Mungu na hapana kwa nafsi zetu wakati ule mapenzi yetu na ya Mungu yanapingana. Yesu aliwaambia wafuasi wake kwamba iwapo walikuwa wanataka kumfuata, itawalazimu kubeba msalaba wao kila siku.

Ili kumfuata Yesu na kuwa kama yeye, tunachagua kusahau kuhusu yale tunataka—mipango yetu, kufanya vile tunataka—na badala yake kumtumainia kutuonyesha mapenzi yake juu yetu. Mapenzi yake hutuongoza katika furaha kuu na kuridhika.


Wewe ni Balozi wa Mungu—mwakilishe vizuri!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon