
Yesu akajibu, akawaambia, hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwaminini yeye aliyetumwa na yeye. YOHANA 6:29
Ninafikiri sisi wote tunajua—lakini tunahitaji kukumbushwa kila mara—kwamba Mungu anatamani watu wenye shukrani, sio watu wa kunung’unika, kulalamika na kutafuta makosa.
Inavutia kugunda kwamba tunaposoma historia ya taifa la Israeli, aina hii ya tabia ilikuwa shida kubwa ambayo iliwasababisha kuzunguka jangwani kwa muda wa miaka 40 kabla ya kuingia katika Nchi ya Ahadi. Tunaweza kuiita kwa majina mengine lakini Mungu aliiita “kutoamini.”
Nia ya Mungu ni kwamba, ikiwa watu wake kweli wanamwamini basi hata kitu gani kifanyike maishani watajua kwamba yeye ni mkubwa vya kutosha kukishughulikia na kukigeuza kufanya kazi kwa wema wao. Maneno ya imani hujazwa na matarajio ya furaha, na sio manung’uniko, kutafuta makosa, na kulalamika. Furaha na amani ni matokeo ya moyo wa shukrani na kuamini.
Sala ya Shukrani
Baba, ninakushukuru kwamba unanikumbusha kuna baraka katika moyo wenye shukrani unaoamini. Nisaidie kukuamini hata kama hali zinazonizunguka si nzuri. Ninajua utanipa kila ninachohitaji.