Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. 1 YOHANA 4:10
Biblia ni rekodi ya neema na upendo wa ajabu wa Mungu. Mashujaa tunaopendezwa nao walikuwa watu tu kama sisi. Walishindwa sana wakati mwingine, ilhali walipata upendo, kukubaliwa, msamaha na rehema kama vipaji vya bure kutoka kwa Mungu. Upendo wake uliwavuta katika uhusiano wa karibu naye, ukawawezesha kufanya mambo makubwa, na kuwafundisha kufurahia maisha yao.
Tunaweza kushukuru kwamba vile tu walivyokubalika, tunaweza kukubalika pia. Mungu haidhinishi dhambi, lakini anawapenda watenda dhambi na ataendelea kufanya kazi ndani yetu hadi tufikie mabadiliko chanya.
Usiharibu wakati ukiishi na hofu kwamba Mungu ana hasira nawe. Shukuru kwamba unaweza kupokea upendo wa ajabu wa Mungu na kujua kwamba hajasikitishwa nawe bora tu unaendelea kumwamini. Imani yako humpendeza (tazama Yohana 6:28–29). Mungu anatupenda kwa sababu amechagua kutupenda na sio kwa sababu tunastahili. Shukuru leo kwamba unapendwa bila masharti!
Sala ya Shukrani
Ninakushukuru, Baba, kwamba unanipenda na kunikubali. Ninaweza kuangalia ndani ya Neno lako na kuona kwamba ulitumia wanawake na wanaume ambao walikuwa na kasoro na ambao hawakuwa wakamilifu. Ikiwa uliwatumia, naona unaweza kunitumia mimi pia.