Nguvu za Kupanda Mbegu

Nguvu za Kupanda Mbegu

Msidanganyike Mungu hadhihakiwi kwa kuwa chochote apandacho mtu ndicho atakachovuna. WAGALATIA 6:7 BIBLIA

Kuna furaha kubwa na faida katika kanuni ya kupanda mbegu. Ukiwapa wengine, Bwana hukubariki pia—pokea baraka zake kwa moyo wa shukrani.

Nimejifunza kufurahia kupanda mbegu mbalimbali. Ninapenda kuwapa walio na mahitaji na kusaidia kuwaleta kwenye kiwango kipya cha furaha, na pia ninapenda kuwapa wale ambao wanafurahia kiwango cha maisha ambayo ningependa kuwa nayo.

Ukitaka huduma yako kukua, tafuta huduma zingine chache kubwa unazoheshimu na upande ndani yake. Ukitaka ndoa yako ipate uponyaji, panda katika maisha ya mtu ambaye ana ndoa nzuri, huku ukiachilia imani yako na mbegu kwa mavuno katika eneo hilo. Ukitaka kufanya kazi kikamilifu zaidi katika tunda la Roho, tafuta mtu ambaye amekomaa katika eneo hilo kukuliko na upande katika maisha yao.

Kwa kweli uwezekano huo hauna mwisho. Ukianza kutumia ulicho nacho kuwa baraka kwa wengine, kisima chako hakitawahi kukauka.


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwamba kuna mavuno, au matokeo kwa kila mbegu ninayopanda. Ninaomba kwamba ninapobariki wengine na kuwekeza katika maisha yao, utafanya mengi zaidi na mbegu hiyo kuliko vile ningefanya nikiwa peke yangu. Asante kwa kuwa kuwapa wengine kunaweza kuwa baraka katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon