Tafuta Karama za Roho

Basi pana tofauti za karama, bali Roho ni yeye yule (1 WAKORINTHO 12:4)

Karama za Roho zinaweza kuwa ngumu za kueleza kwa sababu zinatumikishwa katika ulimwengu wa kiroho. Katika siku chache za ibada zilizopita, ninatumaini na kuomba kwamba nimefanya kazi ya kutosha ya kuzieleza pamoja na kueleza zinavyotumika kimsingi. Kuna mengi ya kusemwa kuhusu mada ya karama za kiroho na ninakuhimiza kusoma vitabu vizuri ambavyo vinaeleza mada ya karama za Roho Mtakatifu kusudi jema.

Tunapotumika katika ulimwengu wa kiroho, tunahitaji kuwa waangalifu lakini sio kuogopa. Shetani hupeana karama potovu lakini tunaweza kuwa katika njia iliyo sawa kupitia kwa maombi na kutafuta ukweli kutoka kwa Neno la Mungu.

Ninakuhimiza pia kuanza kuomba kuhusu karama za Kiroho. Mwombe Mungu azitumikishe hizo karama ndani yako na kuziruhusu kutiririka kupitia kwako vile anavyopenda.

Kuruhusu karama za Roho kufanya kazi kupitia kwetu hutusaidia katika maisha yetu ya kila siku na kudhibitisha nguvu na wema wa Kristo anayeishi ndani yetu kwa wasioamini. Karama za Roho Mtakatifu zinapotumikishwa katika maisha yetu, tunaakisi utukufu wa neema ya Mungu ambayo imetawazwa juu yetu ambao tunahitaji neema ya Mungu kuliko kitu kingine chochote.

Tafuta kutumika katika karama za Roho kwa ajili ya kuinuliwa kwako na kwa wema wa wengine. Unapotafuta karama, usisahau kutafuta haswa kutembea katika upendo kwa sababu upendo ndio karama kubwa kwa zote.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Karama za Roho Mtakatifu zinafaa kuwa sehemu ya kawaida ya maisha yako ya kila siku.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon