Ushirika: Mahali Pa Siri

Hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; tumeokolewa kwa neema (WAEFESO 2:5)

Kuwa na ushirika na Mungu hutupa maisha. Unahuisha; kutia nishati betri zetu, halikadhalika. Tunaimarishwa kupitia kwa umoja na ushirika na Mungu- hodari kabisa kupinga mashambulio ya adui wa nafsi zetu (soma Waefeso 6:10-11).

Tunapokuwa na ushirika na Mungu, tuko katika mahali pa siri ambapo tumekingwa kutokana na adui. Zaburi 91:1 inazungumza kuhusu mahali hapa na kutuambia kuwa wanaokaa huko watamshinda kila adui: “Aketiye mahali pa siri pake aliye juu atakaa katika uvuli wake Mwenyezi [Ambaye hakuna adui anayeweza kupinga nguvu zake].”

Ninaamini mahali pa siri ni uwepo wa Mungu. Tunapokuwa katika uwepo wake, tukiwa na ushirika naye, tunakuwa na amani yake. Shetani huwa hajui tu la kufanya na aaminiye anayesalia kuwa imara pasi kujali hali zilivyo. Jambo hili ni gumu kufanya wakati mwingine, lakini huwa tunavuta nguvu za kuwa imara tunapokuwa na umoja na ushirika na Mungu kupitia kwa Roho wake.

Ushirika na Mungu huchukua muda, lakini ni wakati ambao hutumiwa vizuri. Unakuimarisha ili usiharibiwe na changamoto usizotarajia. Mithali 18:14 inasema, “Roho ya mtu itastahimili udhaifu wake.” Usingoje hadi uwe na matatizo ndipo uwe na nguvu; kuwa na nguvu!

NENO LA MUNGU KWAKO LEO: Haijalishi kinachokukabili maishani sasa hivi, kupitia kwa Yesu una ushindi!  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon