Kumtamani Mungu zaidi ya baraka zake

Kumtamani Mungu zaidi ya baraka zake

Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. Waebrania 13:5

Ni wangapi kati yetu wanaweza kusema kweli, “Sina wivu kwa mtu mwingine au nikwazwe na kile wengine wanacho. Ikiwa Mungu aliwapa, basi nataka wafurahie “? Neno linasema Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; (Waebrania 13: 5). Ninaamini Mungu anatujaribu kuona kama tutaishi kwa andiko hili.

Kuna nyakati ambazo ataweka mtu mbele yetu ambaye ana hasa tunachotaka-ili kuona jinsi tutakavyojibu. Mpaka tuweze kupita mtihani wa “Ninafurahia kwa sababu wewe ni mbarikiwa”, hatuwezi kamwe kuwa na zaidi ya yale tuliyo nayo sasa.

Ikiwa umemwomba Mungu kitu na hajakupa bado, haimaanishi kwamba hataki kukupa. Anataka tu kuhakikisha kwamba unajiondoa wivu na kumfanya awe kipaumbele cha juu.

Mungu anataka sisi kufanikiwa kwa kila njia. Anataka watu kuona wema Wake na jinsi Yeye anatujali. Lakini tunapaswa kumtamani Mungu zaidi kuliko tunavyotaka baraka zake.


OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, nataka Wewe unionyeshe sehemu za maisha yangu ambapo nimejishughulisha na wivu na tamaa, na kunisaidia kupanga upya vipaumbele vyangu. Ninataka kukutamani zaidi kuliko baraka zako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon