Maombi Rahisi ya Kuamini

Maombi Rahisi ya Kuamini

Nanyi mkiwa katika kusali, [msipayuke-payuke kwa kurudiarudia maneno yaleyale mara kwa mara] kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. —Mathayo 6:7

Sikuridhika na maisha yangu ya maombi kwa muda wa miaka mingi. Nilijitolea kuomba kila asubuhi, lakini kila wakati nilihisi kwamba kulikuwa na tatizo. Mwishowe nikamwuliza Mungu tatizo lilipokuwa, na akajibu katika moyo wangu kwa kusema “Joyce, huhisi kwamba maombi yako ni mazuri inavyostahili.” Sikuwa nafurahia maombi kwa sababu sikuwa na hakika kwamba maombi yangu yalikubalika.

Mara nyingi huwa tunajifunga katika sheria zetu binafsi kuhusu maombi. Wakati mwingine tunajaribu kuomba kwa muda mrefu, kwa sauti ya juu, au kwa madoido hadi tunakosa kuona ukweli kwamba maombi ni mazungumzo tu na Mungu. Urefu au sauti ya juu na ufasaha wa lugha ya maombi yetu si muhimu. Vipengele muhimu pekee kwa maombi yetu ni unyofu wa mioyo yetu na uhakika kwamba Mungu anasikia na atatujibu. Tunaweza kuwa na uhakika kwamba hata tukisema kwamba, “Mungu nisaidie,” anasikia na atajibu. Tunaweza kumtegemea Mungu kuwa mwaminifu kufanya vile tulivyomwambia afanye bora tu maombi yetu yawe yanalingana na mapenzi yake.


Maombi rahisi ya kuamini huja moja kwa moja kutoka moyoni na kwenda moja kwa moja katika moyo wa Mungu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon