Toka Utukufu hata Utukufu

Toka Utukufu hata Utukufu

Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho. —2 WAKORINTHO 3:18

Unajiona vipi?

Unaweza kujichunguza kwa uaminifu pamoja na tabia zako na ukose kujihukumu? Unaweza kutazama kwa uaminifu umbali ambao bado unahitaji kwenda, lakini pia umbali ambao umetoka?

Katika 2 Wakorintho 3:18, Paulo alisema kwamba Mungu hutubadilisha “toka kiwango kimoja cha utukufu hata kingine.” Kwa maneno mengine, mabadiliko ndani yetu binafsi hufanyika kwa viwango, na hata yaliyo katika hali zetu, hufanyika katika viwango. Ulipo sasa hivi sipo utakapomalizia.

Iwapo umezaliwa upya, basi uko mahali katika njia ya wenye haki. Huenda usiwe mbali kama ambavyo ungependa kuwa, lakini shukuru Mungu uko njiani. Furahia utukufu tuliomo sasa hivi na usishikwe na wivu kuhusu mahali ambapo huenda wengine wako, au uhukumike kuhusu ulipo. Pengine hatutaweza kwenda kwenye kiwango kingine cha utukufu hadi tujifunze kufurahia ule tuliomo kwa sasa.


Usijikazie sana. Mungu anakubadilisha siku baada ya nyingine na kukuvuta karibu zaidi naye.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon