Kutumainia Mema

Kutumainia Mema

. . . Maana kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake. —MATHAYO 12:34

Mtu aliye karibu na Mungu huwaza mawazo mazuri yanayoinua na kujenga kuhusu watu wengine na pia kujihusu pamoja na hali zake.

Unainua wengine kwa maneno yako kwanza kama umekuwa na mawazo ya mazuri kuhusu huyo mtu. Kumbuka kwamba kilicho moyoni mwako kitatokea mdomoni (Mathayo 12:34). Mawazo na maneno ni vyombo au silaha za kubeba uweza wa kujenga au kubomoa (Mithali 18:21). Hii ndiyo kwa sababu ni muhimu kufanya “kuwaza upendo” kidogo kwa kukusudia.

Ninakuhimiza kuwatumia watu mawazo ya upendo. Nena maneno ya kuhimiza. Tembea na wengine na uwahimize kuchuchumilia mbele katika maisha yao ya kiroho. Nena maneno ambayo yanawafanya wengine kuhisi vizuri zaidi na uwahimize na kuwatia nguvu.

Kila mtu ana shida za kutosha tayari. Hamna haja ya kuongezea dhiki zao kwa kuwararua. Tunaweza kujengana kwa upendo (1 Wathesalonike 5:11). Upendo wakati wote huamini mazuri kwa kila mtu (1 Wakorintho 13:7).


Tunaishi kwa utiifu wa Neno la Mungu wakati ambao mawazo yetu, matendo na mielekeo inafungamana na kile linachosema.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon