Aketiye mahali pa siri pake aliye juu atakaa katika uvuli wake Mwenyezi. ZABURI 91:1
Njia nzuri ya kuwa salama dhoruba inapotokea ni kujikinga. Usipotafuta kinga, huenda dhoruba ikakudhuru.
Neno la Mungu linatufundisha jinsi ya kujikinga tunapokabiliana na dhoruba za kiroho za maisha. Mahali pa kwanza unapohitaji kukimbilia dhoruba inapogonga katika maisha yako ni mahali pa siri pa Aliye juu, uwepo wa Mungu. Tafakari juu ya Neno lake; omba, mwabudu; mshukuru na umwambie kwamba unamwamini hata upepo wa majaribu unapovuma. Hizi ndizo nidhamu za kiroho, hakuna adui anayeweza kuzipinga. Ukijizoesha desturi hizi, kwa kweli utajenga kuta za kiroho za kinga itakayokuzunguka. Kuta hizi zitakupa kinga na kukuwezesha kusimama imara katikati ya dhoruba.
Sala ya Maombi
Bwana, ninakushukuru kwamba wewe ni kinga yangu katika dhoruba. Matatizo ya dunia yakija kwangu, sina haja ya kuogopa kwa sababu uko nami. Ninaamini kwamba utatuliza dhoruba zilizo katika maisha yangu na kunipitisha salama ndani yake. Nashukuru kuwa hutaniacha wala kunipungukia (tazama Waebrania 13:5).