Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, ambao hautatikisika, wakaa milele. ZABURI 125:1
Maana mojawapo ya neno hofu ni “kutoroka,” kwa hivyo tukitumia neno “usihofu,” kwa maana halisi tunasema, “usikitoroke kinachokutia hofu.” Kumbuka, huhitaji kufanya hivyo kwa nguvu zako mwenyewe—Mungu yuko nawe. Unaweza kusonga mbele ukiwa na hakikisho lenye shukrani ndani yake.
Hata hali ikiwaje, kabiliana nayo; usiitoroke. Usijaribu kujificha kutokana nayo; kutana tu nayo ana kwa ana, hata kama unahisi usifanye hivyo. Kila mwanamume au mwanamke ambaye aliwahi kupewa nafasi ya kufanya kitu kikubwa alilazimika kukabiliana na hofu. Utafanya nini unapojaribiwa kuogopa? Je, utatoroka, au utasimama imara, ukishukuru kuwa Mungu yuko nawe?
Sala ya Shukrani
Nikiwa katika hali ambayo ninaanza kushikwa na woga, nisaidie, Baba, kusimama imara katika nguvu zako. Ninashukuru kuwa sihitaji kutoroka. Ninaweza kusimama nikiwa na nguvu nikijua kuwa hofu haina udhibiti juu ya maisha yangu.